Soko la uchambuzi limekuwa shallow mno

Soko la uchambuzi limekuwa shallow mno

 

Ukiacha hasira na lugha kali aliyotumia mzee mzima @harmonize_tz kuna ukweli mchungu ambao wachambuzi inabidi waumeze.


Soko la uchambuzi limekuwa shallow mno wakati wasanii wanavuja jasho na kuwekeza mamilioni, uchambuzi  umebaki wa dakika mbili bila data, bila research ya soko na mara nyingi ukiendeshwa kwa hisia binafsi.


Andiko la Konde linalosema "hamtoona hela zangu tena" linaanika siri na tuhuma nzito hadharani ya tasnia hiyo. Ni kama wanakuwa wepesi mno kununuliwa ili kuendesha ajenda maalumu, kwa mujibu wa Harmo hata yeye inaonekana  alishawamwagia mikwanja. Uhusiano huu wa kimaslahi unaua uhuru wa mawazo.


Mwisho Harmonize anachofanya ni kujenga ukuta kulinda ubunifu wake (Intellectual Protection). Ni kama wasanii wakubwa sasa hivi wamechoka kuhukumiwa na watu ambao hawajui hata muundo wa kiuchumi wa muziki wa sasa. Huu ni ujumbe kuwa kama hufanyi utafiti wa kina na huna data kabla ya kuongea basi kausha huna sifa ya kupima jasho la mtu mwingine.


Japo mwamba hajawasilisha hoja hii kwa lugha ya kistaarabu, lakini amefungua code nyeti ya mapinduzi. Kama tasnia ya uchambuzi Bongo isipo-change wasanii na mashabiki wao wata-stop kuwaheshimu na watabaki kuwa wasoma udaku badala ya kuwa washauri wa kimkakati wa kukuza biashara ya muziki.

Chapisha Maoni

0 Maoni