MIMI SIYO MIKALLA, MIKALLA ALIFARIKI TANGU 2009;_ LUCKIYA.

MIMI SIYO MIKALLA, MIKALLA ALIFARIKI TANGU 2009;_ LUCKIYA.

 

MIMI SIYO MIKALLA, MIKALLA ALIFARIKI TANGU 2009;_ LUCKIYA.

Baada ya siku za karibuni kuzuka tetesi kuwa Mikalla yupo hai na amerejea nchini Tanzania kisha kujiunga Instagram baada ya kutoka Marekani ambako alikuwa anasoma, kila mtu alizungumza lake, wakiwemo wasanii walioigiza naye kwenye tamthiria ya Jumba la Dhahabu iliyovuma miaka hiyo, wengine wakasema walionana naye miezi kadhaa huko nyuma, wengine wakasema ameolewa na wengine wakasema alishafariki mda mrefu.

Ilikuwa ni ngumu kupata mtu wa kumuamini, maana kila mtu alikuwa anaongea lake, wiki iliyopita mwanadada Luckiya, ambaye anatajwa kuwa ndiye Mikalla aliibuka na kueleza kinagaubaga chote juu ya sakata hilo, Luckiya amesema yeye siyo Mikalla, yeye ni mdogo wake na Mikalla na wameachana miaka mingi sana.
Akijibu maswali mbalimbali Luckiya amesema yeye na familia yake wanawashanga wanaosema Mikalla yupo hai kwani Mikalla alishafariki mda mrefu tangu mwaka 2009, alifariki kwa ajali ya gari akiwa masomoni nchini Marekani alikokuwa ameenda kusoma.

"Baada ya kuoneka kwenye filamu ya Kanumba ya "the lost twins" baba yangu hakupendezwa na kitendo hicho, hakutaka aendelee kuigiza alitaka asome hivyo alichokifanya aliamua kumpeleka nchini Marekani kwa masomo, lakini alikaa miezi minne tu akafariki kwa ajali ya gari ambapo gari yao iligongwa na treni ya umeme, walikuwa wanatoka klab na wenzake, miili yao iliharibika vibaya sana kiasi cha kutotambulika"; amesema Luckiya.

"Ilimbidi baba afunge safari hadi Marekani kwenda kupima DNA maana walisagwasagwa haikuwa rahisi kutambua kama huu mwili ni wa mtanzania au mnigeria, baada ya kuletwa Tanzania mwili wake ulienda kuzikwa nyumbani kwetu mkoani Kilimanjaro kwenye makaburi ya kifamilia".


Chapisha Maoni

0 Maoni