Msanii Staa wa Bongofleva Harmonize
amesema kuna vijana wengi wanamfuatilia
hivyo ni jukumu lake kuhamasisha suala la
usafi jijini Dar es Salaam, Harmonize amempongeza pia Rais Samia Suluhu
Hassan kwa jitinada anazo fanya ili kuifanya Tanzania kuwa bora.
Harmonize ambaye ni Balozi wa Usafi na
Uhifadhi wa Mazingira Mkoa wa DSM,
ameyasema hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa
wa DSM, Amos Makalla wakati wa uzinduzi
wa kampeni ya usafi. "Ningependa kuwahimiza vijana kwamba usafi ni suala letu la msingi, na najivunia kuwa kati ya vijana wanaohimiza usafi kwanini haki yetu ya msingi" Harmonize. Mbali na Harmonize, Wasanii wengine waliojitokeza katika uzinduzi wa Kampeni hiyo ni Alikiba, Steve Nyerere pamoja na Viongozi wengine wa Kiserikali wakiwemo Wakuu wa Wilaya.



0 Maoni