Kampuni ya TAXI za mtandaoni ya UBER
imesema itawaruhusu Watumiaji wake wa
Ontario, Canada kuagiza bangi kupitia APP
hiyo upande wa Uber Eats ambao hutumika
kuagiza vyakula na vinywaji. Ni zaidi ya miaka mitatu baada ya Canada kuhalalisha bangi kwa matumizi ya starehe ikiamini kutasaidia Watu kununua bangi salama na halali hivyo kusaidia kukabiliana na soko haramu la chinichini ambalo bado linachangia zaidi ya 40% ya mauzo yote ya
bangi zisizo za matibabu kitaifa. Uuzaji wa bangi nchini Canada utafikia dola bilioni 4 mnamo 2021 na unatabiriwa kukua hadi $ 6.7 bilioni mnamo 2026 kwa mujibu wa data kutoka kwa kampuni ya utafiti ya
tasnia ya BDS Analytics. Uber imeingia makubaliano na kampuni ya TOKYO SMOKE ambayo inamiliki maduka yauzayo bangi sehemu mbalimbali Nchini Canada ambapo Waagizaji watatakiwa kuthibitisha umri wao na kuchukua oda zao



0 Maoni