Facebook imebadilisha jina la kampuni hiyo na sasa itatambulika kama META ambapo Mwanzilishi wake Mark Zuckerberg amesema "Nimekuwa nikifikiria sana kuhusu utambulisho wetu tunapoingia kwenye ukurasa huu mpya, Facebook ni mojawapo ya bidhaa zinazotumika sana katika historia ya dunia, ni chapa maarufu ya media ya kijamii lakini haikuwa ikijumuisha kila kitu tunachofanya bali META itajumuisha"
#
"Leo tunaonekana kama kampuni ya mitandao ya kijamii lakini katika DNA yetu sisi ni kampuni inayounda teknolojia ya kuunganisha Watu ambapo Metaverse ni mstari unaofuata kama vile mitandao ya kijamii ilivyokuwa tulipoanza, jina hili limetokana na neno la Kigiriki meta ambalo linamaanisha 'ZAIDI' na kwangu mimi inaashiria kwamba daima kuna zaidi ya kujenga" ——— Mark Zuckerberg.



0 Maoni