Album ya msanii Wizkid toka Nigeria, “Made in Lagos” Deluxe Edition yenye hitsong kama Essence Remix, imefanikiwa kufikisha jumla ya streams Bilioni Moja (1B). Ilitoka Agosti 27, 2021 (Deluxe Edition).
“Made in Lagos” imefikisha jumla ya streams hizo ikiwa ni mjumuisho wa streams zote za (Deluxe Edition) katika Platform mbalimbali za muziki duniani kama Apple Music (322.75 M), Spotify (229.33 M), Youtube (227.82 M), Audiomack (178.25 M), Boomplay (40.17 M) na Pandora (20.1 M).
WizKid ambaye kwasasa yupo nchini Marekani kwenye ziara yake ya kimuziki ya “Made In Lagos Tour”, aliyoianza Septemba 10 mwaka huu, anaendelea pia kuumiza kwa kupata idadi kubwa ya mshabiki kwenye show zake.



0 Maoni