Staa wa Bongo Fleva, Marioo, amebeba tuzo ya Best Male East Africa katika tuzo za African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) 2026, zilizofanyika Septemba 12, 2026, Dallas, Texas Nchini Marekani.
Marioo alikuwa akiwania tuzo hiyo dhidi ya Wasanii wengine wakubwa wa Afrika Mashariki, wakiwemo Diamond Platnumz, Juma Jux, Mbosso na Barnaba kutoka Tanzania, Bien wa Kenya, Eddy Kenzo na Joshua Baraka wa Uganda, Lij Michael wa Ethiopia pamoja na Single Dee wa Sudan Kusini.
Ushindi huo unakuja katika usiku ambao Marioo pia alikuwa miongoni mwa Wasanii wa Tanzania waliotarajiwa kutumbuiza kwenye AFRIMMA Music Fest, iliyofanyika Annette Strauss Square, Dallas.
Tuzo za AFRIMMA hutambua Wasanii, nyimbo, maonesho na Wadau wengine wenye mchango katika ukuaji na ushawishi wa muziki wa Afrika.
📸#Instagram
📰By #MillardAyoUPDATES





0 Maoni