TV Series ya 'Squid Game' inayofanya vizuri kwenye Netflix

TV Series ya 'Squid Game' inayofanya vizuri kwenye Netflix


 TV Series ya 'Squid Game' inayofanya vizuri kwenye Netflix kwa sasa imetajwa kusababisha ongezeko la Watu wanaojifunza lugha ya Kikorea katika maeneo mbalimbali duniani ambapo App ya kujifunzia lugha mbalimbali ya Duolingo imesema Watumiaji wapya zaidi ya milioni 7.67 walijiunga na App hiyo na kujifunza Kikorea baada ya Series hiyo kuoneshwa kwa mara ya kwanza Netflix.



Netflix wameitangaza series hiyo kuwa ndio iliyofanya vizuri zaidi katika historia baada ya kupata subscribers milioni 111 ndani ya muda mfupi na inakadiriwa kuingiza USD Milioni 900 kutokana na Watu kuitazama ndani ya muda mfupi.


Chapisha Maoni

0 Maoni